Habari za Mastaa

Ile collabo tuliyokuwa tukiisubiri iko njiani, Mafikizolo na Diamond Platnumz kurekodi “Tell Every One”

on

dia

Baada ya kuweka headlines siku ya jana kwa kufanya collabo na superstaa kutoka Marekani Ne-Yo, staa wa Bongo Flava Diamond Platnumz yupo njiani kuelekea South Africa kufanya ile collabo tuliyoisikia kwa muda mrefu sana na Mafikizolo.

Wimbo unaitwa “Tell Every One” ambao ni sehemu ya kampeni ya The Global Goals, kampeni kubwa ya dunia inayolega kutokomeza njaa, umasikini maradhi na matatizo mengine.

maafiki

Mafikizolo kundi la muziki kutoka South Africa.

Mafikizolo tayari washaingiza sauti zao kali kwenye ngoma hio na sasa ni zamu ya mtu wetu anayeiwakilisha Tanzania Diamond Platnumz kunogesha ngoma hiyo. Kizuri zaidi ni kwamba hata mchezaji mpira wa Real Madridn, Gareth Bale  ni sehemu ya kampeni hiyo kubwa duniani.

Hapa nimezinasa picha na video kutoka Twitter zikiwaonyesha Mafikizolo wakiwa Studio na Gareth Bale akiwa anaongelea kampeni hiyo.

mafikidai

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments