Taasisi ya SmartLab Tanzania ambayo ni mvumbuzi mkuu katika elimu ya kidijitali, ifanya uzinduzi wa Mpango wake mpya wa kutoa mafunzo yanayolenga kuziba pengo muhimu la ujuzi na ufanisi nchini Tanzania.
Uzinduzi huo uliadhimishwa katika warsha yao ya “Founder to Founder”, ambayo ilifanyika Ijumaa, Julai 19.
Warsha hio ilibeba mada kuu ya “Mustakabali wa Kazi: Kuongeza Ustadi na Ujuzi kwa Mafanikio ya kidijitali,” uliwaleta pamoja Waanzilishi, wavumbuzi, wajasiriamali na wanafunzi kujadili mustakabali wa kazi na jukumu muhimu la kuongeza ujuzi katika dunia ya leo
Wakati wa hafla hio, SmartLab walizindua programu yao mpya ya SmartLab Learning, inayolenga kufanikisha wataalamu kusonga mbele katika ajira na kwa wahitimu kuweza kupata elimu itakayowaweka tayari kwa ajira.
Programu hiyo itatoa mafunzo ya ana kwa ana yenye lengo la kuwapa ujuzi wa vitendo na kuwawezesha watu binafsi na mashirika kukua katika mazingira ya ushindani wa kidijitali.
“Programu yetu ipo ili kuziba pengo kubwa la ujuzi lililopo kwa sasa na kuwawezesha watu binafsi na mashirika kufanikiwa katika soko la ajira linalobadilika, hasa kutokana na maendeleo ya kidijitali.” Alieleza Mkurugenzi wa Biashara wa SmartLab, Larry Ayo.
Larry alisisitiza kwamba programu hiyo inalenga kutatua tatizo la maendeleo ya ujuzi, hasa wa kidijitali ambao haujitoshelezi katika ulimwengu wa sasa. Watakapomaliza mafunzo yao, washiriki watapokea vyeti na kupata ujuzi wenye thamani kubwa.
Bwana Larry alisisitiza kwa kusema, “Tunawaalika washikadau wote, wakiwemo viongozi wa makampuni, maafisa wa serikali, waelimishaji na wanafunzi, kushiriki katika safari hii ya mabadiliko ya kidijitali, pia tunawasisitiza kujisajili kupitia https://bit.ly/SmartLabLearning ili waanze kupata mafunzo haya.”
SmartLab imejikita katika kukuza utamaduni wa kukuza maarifa pamoja na kuongeza uvumbuzi usio na mipaka hivyo kupitia shule hizi itasaidia kulea Waanzilishi wa Makampuni, Wabunifu na Watengenezaji wa bidhaa mbalimbali ili kuendelea kuwa mstari wa mbele katika maendeleo ya teknolojia na masoko.
Programu ya SmartLab Learning ilizindua shule tano (5) ambazo ni;
1. Shule ya Waanzilishi (Startup School)
2. Shule ya Ubunifu (Creative School)
3. Shule ya Bidhaa (Product School)
4. Shule ya Teknolojia (Technology School)
5. Shule ya Masoko (Marketing School)