Mix

Sentensi tisa za Ali MUFURUKI baada ya Wagombea Urais wa CCM kutofika kwenye Mdahalo leo June 08 Dar

on

IMG-20150608-WA0032

Leo June 08 2015 kulikuwa na mdahalo wa Wagombea wa Urais TZ ambao wanawakilisha CCM.. Mdahalo ulianza saa moja jioni Hyatt Regency Dar lakini Wagombea wengi hawakufika aliyefika ni Mgombea mmoja tu, Balozi Amina Salum Ali, wapo waliotoa sababu za kutofika lakini wengine hakukuwa na taarifa yoyote.

Ali Mufuruki ni mwenyekiti wa Waandaaji wa Mdahalo huo, hiki ndio alichokisema baada ya kutokea kwa hali hiyo>>>”Tumesikitika kwamba wamejitoa.. Hiki ni kitu ambacho kimetuchukua muda mrefu sana kukiandaa. Sijui na sijapata  nafasi kuzungumza nao nini kimewakuta“>>>

Tarehe 18 kutakuwa na mdahalo wa watu wa UKAWA… Hatuwezi kuwalazimisha kuja, wakiamua kutokuja hatuwezi kufanya chochote“>>>

Mzee Sumaye anauguliwa kwa hiyo hakuwepo hapa mjini… Mheshimiwa Nyalandu alithibitisha kushiriki leo asubuhi lakini ameenda Mbeya kikazi na leo usiku atasafiri kwenda nje ya nchi”>>>

Kinana alifafanua kuhusu hili jambo kwamba kila mtu ana hiari ya kuhudhuria ama kutokuhudhuria. Sidhani kama kuna tatizo kwenye chama… Sijapewa sababu ya hawa ambao hawajahudhuria”>>>– Ali Mufuruki.

Sauti yake nimeirekodi pia na unaweza kuisikiliza hapa.

IMG-20150608-WA0029

IMG-20150608-WA0030

IMG-20150608-WA0031

IMG-20150608-WA0033

IMG-20150608-WA0034

IMG-20150608-WA0039

Balozi Amina Salum Ali, huyu ndie Mgombea pekee aliyefika kwenye mdahalo huo.

IMG-20150608-WA0041

Baadhi ya wageni waliofika wakimsikiliza Ali Mufuruki ambae ni Mwenyekiti wa waandaaji.

IMG-20150608-WA0042

IMG-20150608-WA0043

IMG-20150608-WA0045

Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments