Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Moja ya yaliyondikwa kwenye gazeti la Mtanzania ni ripoti ya utafiti huu wenye kichwa cha habari ‘Mtoto akutwa amekufa juu ya dari ’
#MTANZANIA Mtoto wa miaka mitatu, Ilemela Mwanza aliyepotea kwa saa 48 akutwa amekufa juu ya dari la chumba cha mtu aliyepanga nyumbani kwao pic.twitter.com/2RPS1dkCgp
— millardayo (@millardayo) September 21, 2016
Mtoto Rachel Revocatus (3) wa mtaa wa Nyasaka Center wilayani Ilemela aliyepotea kwa saa 48 amekutwa amekufa juu ya dari la chumba cha Ramdhani Musingi aliyepanga nyumbani kwao mtoto huyo. Habari zinasema mtoto huyo alipotea katika mazingira ya kutatanisha wakati akicheza na watoto wenzake.
Tukio hilo lilitokea juzi saa 4:00 asubuhi baada ya mke wa Musingi kuona damu inachuruzika kutoka juu ya dari la chumba chao.
Aliamua kupanda juu ya ndoo kuchungulia ni nini hasa kilikua kinatoa damu hiyo ndipo alipoona gauni la kitenge alilokua amevaa mtoto Rachel aliyepotea jumamosi iliyopita saa 4:00 asubuhi.
Akisimulia mkasa huo mama mzazi wa Rachel, Angelina James alisema aligundua mwanae alikua amepotea september 17 mwaka huu mchana alipomtafuta kwa ajili ya chakula cha mchana.
Mama huyo alisema aliwauliza wapangaji pamoja na watoto wenzake waliokua wakicheza nae kama walikua wamemuona.
Alisema baada ya kutofanikiwa kumuona saa 9:00 alasiri alikwenda kwa uongozi wa mtaa huo kutoa taarifa kama mtu ataonekana na mtoto asiye wake aulizwe, vilevile alitoa tangazo msikitini na kanisani juzi kuhusu kupotea kwa mtoto wake.
Mjomba wa mtoto huyo Johnson Charles, alisema juzi saa 4:00 asubuhi wakati wakiendelea na harakati za kumtafuta Rachel, Musingi alifika nyumbani kwao akawaelezea kuwa mtoto huyo alikutwa juu ya dari la chumba chao akiwa amekwisha kufariki dunia.
Charles alisema mpangaji huyo aliwaeleza kuwa Rachel alifariki dunia akiwa chumbani kwao baaada ya kunaswa na umeme na mdogo wake (jina limehifadhiwa) akaamua kumpandisha juu ya dari kwa hofu.
Unaweza kupitia habari nyingine kubwa kwenye magazeti ya Tanzania September 21 2016
#HabariLEO Wizara ya Elimu imezifuta shule zaidi ya 49 za awali, msingi na sekondari nchini ambazo hazijasajiliwa kuanzia July mwaka jana pic.twitter.com/RGdxANefmm
— millardayo (@millardayo) September 21, 2016
#MWANANCHI Aliyeng'atwa ulimi Singida matatani kwa kujaribu kubaka, polisi wamewashikilia wote kutokana na kila mmoja kumtuhumu mwenzake pic.twitter.com/evKt0D4KMl
— millardayo (@millardayo) September 21, 2016
#MWANANCHI Wakati jumuiya ya Afrika Mashariki ikijipa muda kutafakari mkataba wa EPA, bunge la Kenya limepitisha uamuzi wa kusaini pic.twitter.com/4145BENtXl
— millardayo (@millardayo) September 21, 2016
#MWANANCHI UTAFITI: Ripoti ya utafiti wa UN imebaini kuwa mfumo wa kodi kidigitali utaongeza mapato ya kodi hadi trilioni 1.1 kila mwaka pic.twitter.com/VdV10ycNLA
— millardayo (@millardayo) September 21, 2016
#MWANANCHI CHADEMA leo kufungua pazia la kutoa fomu za kugombea umeya ktk wilaya za Ubungo na K'ndoni pic.twitter.com/8QcsCP671K
— millardayo (@millardayo) September 21, 2016
#MWANANCHI Wanajeshi Uingereza watua nchini kupambana na ugaidi, kuzuia usafirishaji haramu na kuleta usalama ktk upwa wa bahari ya Hindi pic.twitter.com/3YmzRLDVYl
— millardayo (@millardayo) September 21, 2016
#MWANANCHI Shirika la Nyumba la Taifa 'NHC' limesema baadhi ya wadaiwa tayari wamelipa na wengine wameonyesha nia hivyo hawatatimuliwa pic.twitter.com/H8V0pIBok5
— millardayo (@millardayo) September 21, 2016
#MWANANCHI Wauguzi wa zahanati ya Mnenia Kondoa Dodoma wanatumia jengo la wodi ya wazazi kama makazi baada ya kukosa nyumba za watumishi pic.twitter.com/szjJtRDL2z
— millardayo (@millardayo) September 21, 2016
#MTANZANIA Imeelezwa kwa kipindi cha January hadi August mwaka huu kumetokea ajali 237 za mabasi na kusababisha vifo vya watu 254 pic.twitter.com/TcmZqs1V4X
— millardayo (@millardayo) September 21, 2016
#MTANZANIA TFDA inahitaji bil 4.5 kwa miaka mitatu kukabiliana na tatizo la sumu kuvu ambalo hadi sasa limesababisha vifo vya watu 17 nchini pic.twitter.com/lOSxNAqdUH
— millardayo (@millardayo) September 21, 2016
#MTANZANIA CUF wamesema wapo tayari kugharimia matibabu ya katibu mkuu wa chama chao Maalim Seif Sharif Hamad pic.twitter.com/IqViuxzzWy
— millardayo (@millardayo) September 21, 2016
#MTANZANIA Mahakama ya Kisutu DSM imemwamuru Tundu Lissu kujieleza kwa nini asifutiwe dhamana kwa tabia ya kuchelewa na kutofika mahakamani pic.twitter.com/og2Lae67OJ
— millardayo (@millardayo) September 21, 2016
#JamboLEO Walimu 62 msingi na sekondari Mwanza wamesimamishwa kwa tuhuma za kuiba mil 132.5 za elimu bure na kusajili wanafunzi hewa 5,559 pic.twitter.com/wOXq0kniiU
— millardayo (@millardayo) September 21, 2016
#JamboLEO Jiji la Dar es salaam kukusanya bil 60 za mapato kwa mwaka baada ya kufanya maboresho ya mfumo wa habari wa kijiografia 'GIS' pic.twitter.com/Fs7TUHyohn
— millardayo (@millardayo) September 21, 2016
#HabariLEO Wizara ya Elimu imezifuta shule zaidi ya 49 za awali, msingi na sekondari nchini ambazo hazijasajiliwa kuanzia July mwaka jana pic.twitter.com/RGdxANefmm
— millardayo (@millardayo) September 21, 2016
#CHAMPIONI Pamoja na kufanikiwa kupata timu Oman na kuachana na Azam taarifa zinaeleza Kipre Tchetche ametoweka nchini humo pic.twitter.com/VCbnXPeZ0a
— millardayo (@millardayo) September 21, 2016
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI KUTOKA AYO TV SEPTEMBER 21 2016? UNAWEZA KUIANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI