fB insta twitter

Msajili asema Rais Magufuli hajazuia Siasa, afafanua alichomaanisha

on

Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter>>>@millardayo na Zote nakusogezea hapa chini.

Moja ya habari iliyoripotiwa ni hii kutoka gazeti la HabariLEO yenye kichwa cha habari ‘Magufuli hajazuia siasa’

Gazeti la HabariLEO limeripoti kuwa Msajili wa vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi ametetea kauli ya Rais John Magufuli kuhusu kufanya siasa wakati huu na kwamba alichotaka kiongozi huyo wa nchi ni ushirikiano kutoka kwa wanasiasa wenzake ili kuwaletea maendeleo kwa wananchi.

Kupitia gazeti hilo amesema Rais Magufuli katika kauli yake ile hakumaanisha kuzuia shughuli za siasa nchini isipokuwa alielezea kuwa hatakuwa tayari kuona siasa nchini zinakwamisha mikakati ya kuwapeleka wananchi maendeleo yao.

Gazeti hilo limemnukuu Jaji Francis Mutungi ambapo amesema……>>>watu wameitafsiri tofauti kauli ya Rais Magufuli, lakini ni kwamba alikua akiomba ushirikiano na wanasiasa wenzake na wadau wote wa siasa kuleta maendeleo, kwa hiyo kabla ya kukosoa kauli ni vyema ukafanya utafiti siyo kuibeba na kuitafsiri kwa mrengo tofauti’

Unaweza kuzipitia hapa chini habari nyingine kwenye magazeti ya leo June 25 2016

ULIKOSA KUANGALIA UCHAMBUZI WA MAGAZETI JUNE 25 2016 AYO TV? UNAWEZA KUIANGALIA VIDEO HAPA CHINI?

 

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB INSTAGRAM YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments