Mix

PICHA 10: Rais Magufuli alivyozindua mpango wa ugawaji madawati nchini

on

Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli July 13 2016 amezindua mpango wa ugawaji wa madawati yanayotengenezwa kutokana na fedha zilizotolewa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kubana matumizi katika bajeti yake.

Uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya Karimjee Dar es salaam ambapo Rais Magufuli amekabidhi madawati 537 kwa mbunge wa jimbo la Ilala Mussa Azan Zungu kwa niaba ya wabunge wa majimbo yote ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar ambayo yatagawiwa idadi hiyohiyo ya madawati kwa kila jimbo.

.

Rais John Magufuli

Madawati hayo 537 ni sehemu ya madawati 61,385 ambayo yametengenezwa katika awamu ya kwanza na yatafuatiwa na madawati mengine 60,000 yatakayogawiwa katika awamu ya pili na yote kwa ujumla yatagharimu shilingi bilioni 4 ambazo zilitolewa na Bunge April 11 2016 baada ya kubana matumizi katika bajeti yake, ikiwa ni kuitikia wito wa Mhe. Rais John Pombe Magufuli.

Mikoa itakayonufaika katika awamu ya kwanza ya ugawaji wa madawati hayo ni Dar es salaam, Pwani, Morogoro, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe, Rukwa, Katavi, Unguja, Pemba na Tanga.

.

Rais wa John Magufuli na Mbunge wa Ilala Mussa Azzan Zungu ambaye aliyapokea madawati kwa niaba ya Wabunge wa majimbo mbalimbali nchini.

Rais Magufuli amesema baada ya kuanza kutekeleza ahadi ya kuondoa ada kwa shule za msingi na sekondari, idadi ya wanafunzi waliojiandikisha kuanza darasa la kwanza imeongezeka kutoka wanafunzi 1,282,100 hadi kufikia wanafunzi 1,896,584 sawa na ongezeko la asilimia 84.5.

Hiyo imesababisha upungufu wa madawati 1,400,000 lakini tatizo hilo limetatuliwa kwa kiasi kikubwa ambapo mpaka sasa zaidi ya madawati 1,000,000 yametengenezwa ambapo kwenye sentensi nyingine Dkt. Magufuli amelitaka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Jeshi la Magereza kuongeza kasi katika utengenezaji wa madawati ili yakamilike haraka na kuanza kutumika.

.

Rais John Pombe Magufuli na Wanafunzi wa shule ya msingi Bunge.

.

.

.

.

.

.

.

Rais Magufuli na Mbunge wa Iringa Mjini mchungaji Peter Msigwa

ULIKOSA HII YA JPM KUSEMA HUWEZI KUWA NA EXPERIENCE YA OVYO KWA SABABU HATA WIZI NI EXPERIENCE? BINYEZA PLAY HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments