Magazeti

Lowassa+UKAWA+Safari ya Matumaini? CCM je?, Wamachinga Jangwani? Zisikilize zote.. (Audio)

on

national

Magazeti ya July 29 2015 tayari yako mtaani, yote yakiwa na vichwa vyake vikubwa vya habari. Nimekusogezea zile zote kubwakubwa za leo zilizochambuliwa redioni.

Lowassa yeye na CCM basi, safari ya matumaini yahamia rasmi UKAWA asema CCM sio baba yake wala mama yake, akabidhiwa kadi ya CHADEMA… CCM yasema itabaki kuwa imara Lowassa ajimaliza, waitisha mkutano muhimu na waandishi wa habari leo Dar.

TAKUKURU yadaka Wagombea Ubunge CCM Jimbo la Ukonga kwa tuhuma za rushwa, Vituo vya BVR vyaagizwa kufunguliwa saa moja kamili asubuhi badala ya saa mbili ili kuharakisha zoezi la uandikishaji.

Wafanyabiashara wa maeneo ya Jangwani waagizwa kubomoa vibanda vyao vya biashara… Ajali mbaya ya basi yaua Mapadri wawili Kagera, Kundi la Panya Road wadaiwa kuvamia mitaa ya Kikogo na kupora kwenye vituo vya BVR.

Mradi wa mabasi ya mwendokasi DART umekamilika kwa 90% na unategemea kuzinduliwa mwezi Agosti, ruti ya kwanza itakuwa  Kivukoni kwenda Kimara.

Sauti yote ya uchambuzi wa magazeti @CloudsFM nimekurekodia na kukusogezea hapa chini.


Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments