Top Stories

“Magaidi sasa wana njia zote za urahisi kupanga mipango” Rais Samia

on

“Dunia sasa iko kwenye wimbi la 4 la mapinduzi ya viwanda na linaongozwa na mifumo ya TEHAMA, mawimbi haya yanakuza Ugaidi, Magaidi sasa wana njia zote za urahisi za kuwasiliana na kupeana mipango,Polisi mnatakiwa kuwa tayari kuwaona wanachokifanya”——Rais Samia

“Kesi nyingi zinakwama Mahakamani kutokana na kucheleweshwa kwa upelelezi au kwamba hazina ushahidi hizi tunaita kesi za kubambikizwa, nawapongeza Polisi kwa kuweka ukomo wa upelelezi kufikia miezi 6 kwa kesi ndogo na mwaka mmoja kwa kesi kubwa”———Rais Samia

“Kucheleweshwa kwa upelelezi kunaongeza mzigo mkubwa kwa Serikali kuwaweka Mahabusu Jela, takwimu mpaka Mwezi huu tarehe 22 idadi ya Mahabusu katika Jela zetu ni karibu sawa na Wafungwa, Wafungwa walikuwa 16,542 ila Mahabusu ni 15,194 mpaka juzi”——-Rais Samia

“Mahabusu kuna waliokaa wiki, mwezi,mwaka na kila anayeguswa upelelezi haujakamilika, nitoe wito kesi ambazo mna uhakika upelelezi hautokamilika basi watolewe wakafaidi uhuru wao, na zile kesi ambazo mna uhakika upelelezi utatimia basi uharakishwe”———Rais Samia

“Naomba Polisi mkae na Wadau wengine muangalie uwezekano wa kurekebisha Sheria za kuweka Watu Mahabusu, kwenye Nchi za wenzetu Mtu hakamatwi mpaka upelelezi umetimia, akikamatwa anawekwa Mahabusu siku 3 au 4 tayari Mahakamani anahukumiwa anaendelea”——Rais Samia

“Polisi baadhi yenu mnashutumiwa kwa kutofanya haki kwa Jamii, miezi miwili mitatu nyuma kulikuwa na unyang’anyi wa nyama mlivamia bucha mkachukua nyama za Watu walipolalamika mkasema mmefanya vile kwa Sheria ila ukiangalia kwa undani hakuna Sheria”——Rais Samia

Soma na hizi

Tupia Comments