magari

Hadi kufikia February 2015, hii ndio ilikuwa list ya magari matano makali na gharama kubwa duniani (+Pichaz)

on

Najua katika maisha kila mtu ana dream car yake yaani gari ambayo angependa kumiliki na kutembelea wakati atakapokuwa amepata pesa, gari zipo nyingi sana lakini inategemea na wewe mwenyewe unahitaji gari aina gani? kwa matumizi gani mtu wangu, nimekutana na list kutoka ubergizmo.com ya magari matano ya gharama. Hadi kufikia February 2015 hii ndio list ya magari matano ya gharama.

5- Bugatti Veyron Super Sports ($2.4 million)

Bugatti-Veyron-Super-Sports

Bugatti Veyron Super Sports kwa fedha za kibongo inauzwa zaidi ya Bilioni 5

4- Lykan Hypersport ($3.4 million)

Lykan-Hypersport

Lykan Hypersport bei yake kwa fedha za kitanzania Tsh Bilioni 7

3- Lamborghini Veneno ($4.5 million)

Lamborghini-Veneno

Hii mtu wangu huwezi kumiliki hadi uwe na bilioni 9 za kibongo

2- Koenigsegg CCXR Trevita ($4.8 million)

Koenigsegg-CCXR-Trevita

Inahitaji zaidi ya Bilioni 10 za kitanzania ili uweze kuimiliki mtu wangu.

1- Maybach Exelero ($8.0M)

Maybach-Exelero

Katika list hii Maybach Exelero ndio gari yenye gharama ya juu zaidi inahitaji Tsh Bilioni 17 ili mtu aweze kuimiliki.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwapia ungana na MillardAyo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments