Miongoni mwa zile zilizopewa Headlines kwenye Magazeti ya leo April 01, Mgombea wa chama kikuu cha upinzani Nigeria Muhammadu Buhari ameshinda katika uchaguzi wa Urais nchini humo, Askofu Gwajima aachiliwa kwa dhamana, baadhi ya wafanyabiashara wamendelea kufunga maduka Kariakoo, hukumu ya kesi ya wizi wa fedha za katika akaunti ya EPA, inayomkabili Rajabu Maranda kutolewa Mei 29.
Shirika la nyumba limetakiwa kufanya tathimini ya nyumba wanazojenga kwa ajili ya kuuzwa kwa wananchi, Mjumbe wa kamati kuu CCM Jerry Silaa amesema mfumo wa kumtafuta mgombea wa Urais CCM umepitwa na wakati, EWURA imetangaza kupanda kwa bei ya mafuta ya petroli kuanzia April 04, Kamanda Kova amesema tukio la kuuawa kwa Askari wawili Wilayani Mkuranga lina dalili za ugaidi na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu amefanya mabadiliko ya makamanda wa Mikoa kama njia ya kuimarisha usalama nchini.
Sheria ya makosa ya mitandao huenda ikapitishwa Bungeni leo, katika uchambuzi wa Magazeti kulikuwa na mazungumzo na mtaalam wa masuala ya usalama wa mitandao na uchunguzi wa makosa ya digital, Yusuph Kileo ambae amepongeza hatua ya kuanzisha sheria za kupambana na uhalifu wa mitandao.
88.1 Clouds FM inasikika ukiwa Mwanza.
Bonyeza play hapa chini kusikiliza uchambuzi wa story zote za Magazeti ya leo…
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza>>> twitter Insta Facebook