POWERBREAKFAST ya Clouds FM imefanya uchambuzi wa story kubwa zote za kwenye kurasa za Magazeti TZ, kama ulikuwa mbali na Redio yako basi unaweza kusoma na kusikiliza stori zote zilizosikika hewani leo April 07, hapa.
April 07 ni siku ya KARUME DAY ambayo ni kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa Rais wa kwanza Zanzibar, Abeid Amani Karume, Mwenyekiti wa jumuiya ya wafanyabiashara amesema hakuna dalili za viongozi waliopo madarakani kumaliza mgogoro uliopo kati ya wafanyabiashara na TRA, Mkurungenzi wa taasisi ya Mwl. Nyerere, Joseph Butiku amesema mambo ya msingi yaliyotolewa kwenye Katiba mpya yarejeshwe, Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa amesema haelewi ni kwa nini Serikali imeshindwa kuteketeza meno ya tembo.. iko pia stori ya wagonjwa wanaolazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kondoa kulazimishwa kufanya usafi wodini.
Magaidi watumia mbinu ya kuwapa mafunzo wananchi wa nchi husika ili kurahisisha kupanua mtandao wao, mashine 248 za BVR zimewasili TZ, kwa ajili ya zoezi la kuandikisha wapiga kura, Maaskofu wa Japani wamponya Askofu Gwajima kwa maombi maalumu, wananchi wafanya uharibifu katika treni mpya ya kisasa ya Deluxe, watu watano wamefariki baada ya kupigwa na radi wakiwa Kanisani Geita, waumini wa Kanisa Katoliki jimbo la Mpanda walishindwa kusali baada ya kutokea ugomvi wa kwaya mbili za Kanisa hilo.
104.1 Clouds FM inasikika ukiwa Bukoba.
Bonyeza play hapa chini kusikiliza story zote…
Hakuna Stori itakayokupita mtu wangu,niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza>>> twitter Insta Facebook