Magazeti

Mengine ya bastola ya Gwajima.. Wafuasi wa CUF wapigwa.. TZ na ishu ya ugunduzi gesi… #PBCloudsFM

on

5438674967_d3078c2691_bPOWERBREAKFAST ya Clouds FM imefanya uchambuzi wa story kubwa zote za kwenye kurasa za Magazeti Tz, kama ulikuwa mbali na radio yako basi hapa unaweza kusoma na kusikiliza stori zote zilizosikika hewani leo March 31.

Askofu Gwajima amesema aliagiza bastola kwa ajili ya kujilinda, wasichana 3 wamekamatwa kwa kuhusishwa na ugaidi Kenya yumo Mtanzania, wadau wanaotumia mitandao nchini wamepinga madai yaliyoidhinishwa kuhusu muswada wa sheria ya makosa ya mtandao, wafuasi 25 wa CUF wavamiwa na kupigwa na watu wanaodaiwa kuwa wanachama wa CCM, Serikali imetangaza ugunduzi mpya wa gesi asilia huko Lindi, watu watano wanusurika kifo baada ya ukuta wa jengo walilokuwa wakijenga kudondoka Mwanza, nauli mpya za usafiri wa umma kujulikana mwishoni mwa wiki hii, Zanzibar yakumbwa na uhaba wa Petroli na kuleta usumbufu kwa wananchi.

Kulikuwa na mahojiano  na wafanyabiashara mbalimbali pamoja na Mkurugenzi wa jumuiya ya wafanyabiashara Steven Chamle ambao wamezungumzia mgomo wa wafanyabiashara unaoendelea TZ.

104.1 Clouds FM inasikika ukiwa Bukoba.

Bonyeza play hapa chini kusikiliza story zote…

Hakuna Stori itakayokupita mtu wangu,niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Soma na hizi

Tupia Comments