Uchambuzi wa magazeti redioni @CloudsFM umekupita? Inawezekana hukuzipata zote zilizoweka headlines kwenye kuperuzi na kudadisi asubuhi hii… kama ilikupita hizi ni dakika 20 za zile zote kubwa za leo.
Fedha sherehe za Uhuru December 9 kupanua barabara ya Mwenge kwenda Morocco, ni agizo kutoka Rais Magufuli lengo kupunguza foleni barabarani, Rais Magufuli amuibua Lipumba, Zitto Kabwe asema waliofuja dola Milion 600 Stanbic Bank waadhibiwe.
Panga kali kutua kwa wafanyakazi wa Mashirika ya Umma, ni amri kupunguza mzigo mashirika yasiyozalisha… malipo ya bodi zote sasa kuangaliwa upya, kuanzia sasa Wabunge hakuna kulipwa posho kwenye ziara, Vigogo zaidi TRA mbaroni ni sakata la wizi wa makontena 349 sasa wafikia 12 wengine watakiwa kujisalimisha, Polisi wacharuka.
January Makamba asema Rais Magufuli ameipa pumzi mpya CCM, Rais Magufuli aagiza Wabunge waondolewe kwenye Bodi za Mashirika ya Umma, Baraza zuri la Mawaziri lazidi kusukwa… Chama cha CCM Zanzibar kimekanusha taarifa zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba kimeridhia mgombea wa Urais kwa ticket ya CUF, Maalim Seif kuapishwa na kukabidhiwa nchi.
TRA yaibana mbavu Shirika la mabasi UDA baada ya mabasi 9 ya shirika hilo kukamatwa kwa kosa la ukwepaji kodi.
Sauti yote ya uchambuzi wa magazeti kwenye #PowerBreakfast ipo hapa chini, kusikiliza bonyeza play ikupeleke moja kwa moja.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE