Good Morning mtu wangu ni asubuhi nyingine na kama kawaida lazima tuanze na uchambuzi wa magazeti redioni @CloudsFM… Kama ilikupita hizi ndio kubwa za leo kwenye Kuperuzi na kudadisi.
Watu tisa wakiwemo Mawaziri wawili wa Fedha wa Serikali awamu ya nne ya Rais Mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete wametajwa kushiriki kwenye kashfa ya rushwa wa Tsh Bilion 13 wakati serikali ya Tanzania ilipokopa Dola za Kimarekani milion 600 (shilingi trilioni 1.3) kutoka benki ya Standard ya Uingereza. Ripoti ya Taasisi ya Kuchunguza Makosa ya Ufisadi (SFO) ya Uingereza iliyokuwa inafuatilia kashfa hiyo imewataja maafisa hayo kuwa ni Waziri wa Fedha aliyefukuzwa kazi May 2012, Mustafa Mkulo na Waziri wa Fedha aliyefariki dunia January 2014, Dk. William Mgimwa.
Rais John Magufuli ameombwa kuzuia uagizaji wa nguzo za umeme kutoka Africa Kusini kunakofanya na Shirika la umeme Tanzania, TANESCO kupitia wazabuni ili kumnusuru mamilioni ya fedha za kigeni… Chama cha CHADEMA kimesema hakishitushwi na kasi ya utendaji kazi wa Rais Magufuli kwani amekuwa akitumia kanuni na sera ya chama hicho.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Donald Mbando amesema maduka ya madawa yalipo karibu na hospitali zote nchini hayatafungwa kama inavyodaiwa isipokuwa maduka ya bohari kuu ya dawa, MSD watauza dawa zake kwa gharama nafuu zaidi.
TPA wakomalia wamiliki wa makontena 9 Dar es salaam, wasema watu waliosafirisha makontena hayo na kuyahifadhi sehemu isiyo rasmi wamekeuka Sheria na taratibu kwani nyaraka za kutolea mizigo bandarini hazionyeshi kama makontena hayo yalitakiwa kuhifadhiwa sehemu hiyo. Ukaguzi wa kilichohifadhiwa ndani ya makontena hayo bado unaendelea.
Hapa chini ni dakika 20 za uchambzui wote wa magazeti kwenye #PowerBreakfast, kusikiliza bonyeza play ikupeleke moja kwa moja.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.