Uchambuzi wa magazeti redioni @CloudsFM umekupita? Inawezekana hukuzipata zote zilizoweka headlines kwenye kuperuzi na kudadisi asubuhi hii… kama ilikupita hizi ni dakika 25 za zile zote kubwa za leo.
Makontena yaliyokwepa kodi TRA yafikia 2431, Rais Magufuli amuonya mfanyabiashara anayetaka kumiliki ufukwe wa Coco Beach, Vigogo TRA wakutwa na mamilioni nyumbani, bosi mpya awataka watumishi wote kuzitaja mali zao… Rais Magufuli atoa siku saba kwa wapigaji awaambia wasipolipa kodi ndani ya muda huo wataisoma namba.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jana alifanya ziara nyingine ya kushtukiza Bandarini baada ya kupewa taarifa kuwa kuna makontena 2431 yametolewa bila kulipia ushuru kwenye Bandari Kavu nne ambazo ni JFEAG, DICD, PMM na AZAM na kisha kuwasimamisha kazi watumishi kumi kutokana na makosa hayo.
Shirika la AFIDF imesema kuwa madudu yanayoibuka katika Bandari ya Dar es salaam yatadhibitiwa ikiwa Serikali itafanya maamuzi ya kufufua Shirika la Taifa la Wakala wa Meli, NASACO ili kuhakikisha mizigo yote inayopita Bandarini inaratibiwa kwa usahihi.
Rais Dk. John Magufuli amesema hakuna Mfanyabiashara aliyemchangia kuingia Ikulu ili aweze kusimamia ipasavyo kodi za wananchi kwani alijua akiingia madarakani anakuja kufanya kazi hivyo amewaomba wanafanyabiashara wote kufanya biashara ya kweli na haki na kukemea tabia ya baadhi ya wafanyabiashara kutumia maeneo ya wazi kufanya biashara kutokana na uwezo wao wa kifedha na kusisitiza kuwa kitendo hicho hakitakubalika na Serikali yake.
Serikali imepiga marufuku kwa wamiliki wa Shule Binafsi kupandisha ada za shule kwa mwaka wa masomo unaoanzia January 2016 mpaka pale watakapopata maelekezo kutoka kwa Kamishina wa Elimu.
Sauti yote ya uchambuzi wa magazeti kwenye #PowerBreakfast ipo hapa chini, kusikiliza bonyeza play ikupeleke moja kwa moja.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.