Magazeti

Headlines za siasa.. Ishu ya Mwakyembe na Lowassa kuhusu ujumbe wa mtandaoni, Mazishi ya Mbunge Mwaiposa.. Ziko stori zote hapa

on

On Air

Uchambuzi ambao huwa unafanywa kwenye radio kwa kupitia kurasa za Magazeti ni moja ya vitu vinavokusogezea stori za kubwa karibu na wewe popote ulipo.. kwa sasa ni kama siasa imetawala headlines kwa vile huu ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu TZ.

Ngeleja amesema anagombea Urais TZ ili kupambana na maadui sita ikiwemo Rushwa na Umaskini, amesema mwenye ushahidi wa yeye kuhusika na ESCROW auweke hadharani.. stori nyingine inahusu Makamu wa Rais Gharib Bilal amesema atasimamia maadili kama CCM ikipitisha kugombea Urais wa TZ.

Mtumishi wa CCM, Amos Siantemi amesema Watz wamepoteza imani kwa Serikali na kuamini kuwa CCM haijali wanyonge, amesema akiteuliwa kuwa Rais wa TZ atarudishwa mfumo wa  nyumba kumikumi.

Siasa na headlines zake, nyingine inahusu Waziri Magufuli kuchukua fomu kimyakimya na kusema ataongea na vyombo vya Habari baada ya kumaliza kuzisoma fomu za Urais, atinga Dodoma akiwa na wapambe watatu.. Polisi yaanza msako kubaini walioweka taarifa mtandaoni iliyoonesha Mwakyembe kamchafua Lowassa.

Mwakyembe amesema hajawahi kumchafua Lowassa mitandaoni, asema hizo ni siasa za kitoto.. stori nyingine inahusu Jeshi la Polisi kumshikilia mama mmoja kwa kesi ya kutaka kuiba mtoto Hospitali ya Mwananyamala ili kulinda ndoa yake.. DECI imerudi kwenye headlines, Serikali imesema inamfanya mpango wa kuwalipa walioweka pesa zao DECI.. Viongozi 19 wa CHADEMA wamesimamishwa Geita.

Mazishi ya Mbunge Eugene Mwaiposa kufanyika kesho Dar, pia kuna stori inayohusu watu 150 kukosa makazi kutokana na mvua kubwa kubomoa nyumba Geita.. stori hizo na nyingine utazisikia kwenye sauti hapa.

Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments