Ad
Ad

Magazeti

Rais JK Bungeni, Mapadri kuvamiwa.. Mikoa na Wilaya mpya TZ, Rais UKAWA.. Stori kubwakubwa TZ

on

PowerBreakfastLogo2

 

Inawezekana uchambuzi wa stori za magazeti redioni kupitia @CloudsFM umekupita, story zake ni muhimu zikufikie pia… hapa nimenukuu baadhi ya story na iko sauti ambayo ina stori zote mtu wangu.

Rais Jakaya Kikwete jana amehutubia Bunge la kumi  kwa mara ya mwisho lakini ametangaza kuwa Bunge hilo litavunjwa rasmi mwezi Agosti tarehe 20, UKAWA wamepanga kumtangaza mgombea wao wa Urais kesho.

Rais Kikwete ametangaza kuanzishwa kwa Wilaya 6 mpya, Ubungo na Kigamboni kutajwa kuwa Wilaya mpya huku Songwe ikitajwa kuwa Mkoa mpya, Sheria ya Tume ya walimu yapitishwa jana Bungeni.

Stori nyingine iliyosikika leo, Tanzania yatajwa kuwa miongoni mwa nchi zinazoingiza mapato madogo yanayotokana na Kodi duniani na Serikali yaombwa kutunga Sheria mpya zitakazobana makampuni binafsi katika ukwepaji wa kulipa Kodi nchini.

Kuna stori pia kutoka Mbeya ambayo inahusu Mapadri kuvamiwa na majambazi na kuporwa mali zao wakiwa njiani kuelekea kwenye sherehe za Upadrisho.

Unaweza kuzipatastori zote kwenye hii sauti pia.


Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook naInstagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments