Good Morning mtu wangu, Uchambuzi wa magazeti redioni @CloudsFM umekupita? Kazi yangu siku zote ni kuhakikisha zile zote kubwa za siku zinakufikia, hizi ni baadhi ya stori zilizoguswa kwenye Uchambuzi redioni.
Traffic afukuzwa kazi, anaswa katika video akipokea rushwa, NEC yatoa ratiba ya marudio ya uchaguzi, Uspika CCM ngoma nzito, CHADEMA waanika vigezo viti maalum, Muhimbili hakukaliki, vigogo wajifungia vikaoni kujipanga upa, Mawaziri wamtesa Rais Dk. John Magufuli, sura mpya zatajwa kuingia baraza jipya na msaidizi wa Lowassa mbaroni.
Jeshi la Polisi Katavi wamefanikiwa kuzuia kufungwa kwa ndoa ya watoto kinyume na Sheria, mume akiwa na miaka 17 huku mke akiwa na miaka 14 na licha ya bibi harusi kukataa kuolewa na kutaka kuendelea na elimu yake, baba wa msichana huyo alikataa kwani alikuwa ameshapokea mahali ya ng’ombe 11.
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amempongeza Rais Dk. John Magufuli kwa kitendo cha kupiga marufuku safari za nje ya nchi asema kitendo hicho kitaokoa pesa nyingi za Serikali kwani kila safari ya nje ina gharama yake na kila safari itakayofutwa pesa zake zitaweza kutumika kuendesha shughuli nyingine za Kiserikali.
Benki ya Dunia imetoa taarifa kuhusiana na tatizo la mabadiliko ya tabia nchi, tatizo ambalo limetajwa kuwa kikwazo kikubwa katika kuwakomboa watu katika umasikini na kama hakutakuwepo na mikakati ya haraka, kutakuwa na ongezeko la watu masikini milioni 100 watakaokabiliwa na umasikini mkubwa kufikia mwaka 2030, Tanzania yatajwa kuwa miongoni mwa nchi za jangwani mwa sahara zitakazoathirika na tatizo hili kutokana na kupungua kwa uzalishaji wa chakula na kuongezeka kwa bei za mazao kufikia mwaka 2030.
Jeshi la Polisi Tanga limemfukuza kazi aliyekuwa askari wake wa kikosi barabarani, Anthony Temu wa kituo cha polisi Kabuku wilaya ya Handeni kutokana na kosa la kuomba na kupokea rushwa, taarifa iliyopatikana kupitia mitandao ya kijamii.
Tunaomba radhi kutokana na tatizo la sauti.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE