Magazeti

Hofu ya EBOLA Kigoma.. mengine Kura za Maoni CCM? Waziri Chikawe na msafara wa Lowassa? (Stori +Audio)

on

radio-mikrofon_01

Kwenye stori kubwakubwa nimeziweka karibu na wewe hizi hapa mtu wangu, headlines kubwa zilizobebwa kwenye Magazeti ya Tanzania August 12 2015.

Hofu ya Ugonjwa wa Ebola yatanda Kigoma baada ya mtu mmoja kufariki akiwa na dalili za Ugonjwa huo, Mamlaka ya mawasiliano TCRA imeendelea kuwaonya watu kuhusu matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii hasa kipindi hiki kuelekea Uchaguzi mkuu.

CCM kurudia kura za maoni kesho katika majimbo 5 Tanzania baada ya Kanuni za Uchaguzi kukiukwa… Dk. Wilbroad Slaa akana taarifa zinazosambaa mitandaoni kuhusu kujitoa CHADEMA, amesema hana account ya Twitter.

CCM na UKAWA wamekuwa gumzo…Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mathias Chikawe akanusha fujo kutokea kwenye msafara wa Edward Lowassa asema maandamano hayo kuelekea ofisi za NEC yalikuwa ya amani yaliyofuata utaratibu wa kisheria.

NEC yaionya UKAWA kutangaza matokeo ya Urais na pia imewaonya wanasiasa kutoingilia shughuli zao za Tume… Rais Jakaya Kikwete afanya uteuzi wa balozi mmoja na kubadilisha wengine 2 vituo vya kazi… Stori zoteziko kwenye hii sauti pia niliyorekodi show ya PowerBreakfast @CloudsFM.


PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments