Magazeti

Magufuli kuipeperusha CCM, UKAWA na mgombea wake, BVR yasogezwa mbele Dar<<< Stori Kubwa (Audio)

on

Morning_News

Ni Jumatatu nyingine tena na inawezekana uchambuzi wa magazeti leo Julai 13 umekupita. Nimekusogezea stori zote za magazeti kupitia @Clouds.Fm  zikiwa na baadhi ya stori hizi kubwa.

Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli ateuliwa kuwa mgombea Urais kupitia CCM na ameahidi kutokukiangusha Chama hicho, huku akimteua Samia Suluhu Hassan kama mgombea mwenza.

Ulinzi wa nyumbani kwa Dk. John Magufuli umeimarishwa baada ya kutangazwa kuwa Mgombea Urais kupitia chama cha CCM, Viongozi wa Vyama vya upinzani UKAWA wasema hawatishwi na John Magufuli na wamejipanga kumtangaza rasmi mgombea wao wa Urais kesho.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC imetangaza kusogezwa mbele kwa zoezi la uandikishaji wa kupiga kura kwa Dar es salaam kutoka Julai 16 hadi Juali 22.

Sauti ya stori zote za magazeti kupitia @Power Breakfast iko hapa chini..


Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook naInstagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments