Leo ni siku nyingine tena, na inawezekana uchambuzi wa stori za magazeti leo July 16 2-15 kwenye #PowerBreakfast @CloudsFM umekupita, nimekusogezea stori zote za leo.
Chama cha CUF imetaka viongozi wa chama hicho kusitisha zoezi la kutafuta mgombea Urais kupitia UKAWA mpaka suala hilo litakapojadiliwa kikatiba ndani ya chama hicho siku ya Julai 25.
Viongozi wa dini waandaa maandamano kwa lengo la kumuomba Rais Kikwete kulifanyia mabadiliko Jeshi la Polisi, baadhi ya madereva wa bodaboda wamkana jambazi wa tukio la Stakishari wasema hakuwahi kuwa mwenzao.
Mtu mmoja amenusurika kufa baada ya mguu wake wa kulia kuliwa na fisi akiwa usingizini, mtaro wa maji machafu imekuwa kikwazo Kawe na NEC imetaja mipaka ya Majimbo mapya na mipaka mingine kukamilia baada ya sikukuu za Eid El-Fitr.
Matokeo ya kidato cha sita yametok na kijana Ramadhani Gembe ameongoza mwaka huu.
Sauti ya stori zote hizi iko hapa chini.
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.