Magazeti

Lowassa aiteka Mwanza, Rais Kikwete na wanaohama CCM, kuna uchakachuaji Uchaguzi 2015? (Audio)

on

Monday_Mornings_logo

Ni Jumatatu nyingine tena na magazeti ya August 17 2015 yako mtaani tayari, hizi ni stori zake kubwa nilizozinasa baadhi zikiwa…

Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa asimamisha jiji la Mwanza kwa zaidi ya saa tatu… Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwl. Julius Nyerere, Joseph Butiku asema wananchi wasimchague mtu anayeitaka Ikulu kwa fedha kwani hawafai kupewa uongozi wa nchi.

Dk. John Magufuli asema CCM watashinda na hawaishi kwa matumanini, Kingunge hatarini kutemwa  na CCM… Rais Jakaya Kikwete asema uamuzi wa nani agombee Urais  kupitia CCM ulifanyika kwa pamoja na kufuata taratibu, anayetoka kwenye Chama hicho anafanya hivyo kwa hiari na maamuzi yake.

Mgombea Urais wa ACT Wazalendo kujulikana leo…NEC yasema hakuna uchakachuaji kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 bali matokeo yatakuwa ya usawa kwa vyama vyote.

Uchambuzi wote wa stori zote za magazeti uko kwenye hii sauti niliyorekodi kupitia Power Breakfast @CloudsFM.


PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments