Magazeti

Orodha ya Wabunge CHADEMA.. Kamati ya kampeni CCM? Urais ACT Wazalendo gizani, TADEA je? #PowerBreakfast

on

mor

Kwenye stori kubwa August 19 2015 kuna hizi kubwakubwa mtu wangu ambazo ziligusa pia Uchambuzi wa Redioni.

CHADEMA yatangaza orodha ya wanachama wake watakaogombea Ubunge… Kamati kuu ya CCM yatangaza kamati yake ya Kampeni ya mgombea wao wa Urais Dk. John Magufuli na mgombea mwenza Samia Hassan Suluhu yenye vigogo 32.

Chama cha TADEA kimetoa rai kwa Watanzania wote wenye sifa za kugombea Ubunge, Uwakilishi na Udiwani kujiunga na Chama hicho… Mchakato wa kumpata mgombea Urais umewachanganya ACT Wazalendo na kukilazimu chama hicho kukaa upya vikao kwa ajili ya kumpata Mgombea wao Urais.

Watu 4 wanaosadikiwa kuwa majambazi wavamia wafanyabiashara kwenye kijiji cha Vikonge wilayani Mpanda na kupora mali zenye thamani  zaidi ya Milioni 7… Rais JK awahakikisha wakuu wa nchi za SADC kuwa uchaguzi wa mwaka huu utafanyika kwa haki, uhuru, amani na utakuwa wa mafanikio.

Sauti ya stori zote za uchambuzi wa magazeti ndani ya #PowerBreakfast @CloudsFM nimeirekodi na kukuwekea hapa chini.


PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments