Magazeti

Lowassa na Magufuli kimyakimya? NEC matokeo ni ndani ya siku 3!? Nkurunziza aapishwa!? (Audio)

on

frii

Ni ijumaa nyingine na uchambuzi wa magazeti @CloudsFM umefanyika, ninazo zile zote zilizotawala kwenye vichwa vya habari na kuguswa na Uchambuzi wa Redioni.

Hofu imetanda kwa watumiaji wa magari na mitambo nchini kutokana na taarifa ya uwezekano wa bei ya diesel na Petroli kupanda… Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limewataka viongozi wa Siasa kuacha kuwatumia walezi wao kwenye kampeni za Kisiasa.

Lowassa na Magufuli kurudisha fomu za Ugombea Urais kimyakimya…. James Mbatia asema UKAWA wataendelea kusonga mbele licha ya tofauti na changamoto zao na anayetaka kuondoka kwenye Umoja huo ana haki ya kufanya hivyo bila kuzuiwa na mtu.

NEC yaonya siasa kwenye nyumba za ibada, yawapiga marufuku viongozi wa dini kufanya kampeni za kisiasa kwenye nyumba za ibada… NEC imesema safari hii matokeo ya Urais kutangazwa ndani ya siku 3.

Wagonjwa wa Kipindupindu wafikia 56 Dar es Salaam, Mkuu wa Mkoa wa Dar amewataka watu wa Dar kuacha kusalimiana kwa mikono kwenye kipindi hiki ili Jambazi sugu wa tukio la Sitakishari atajwa.

Moja kutoka Burundi yasema Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza aapishwa ghafla jana kutumikia muhula mwingine wa miaka 5 na hakuna mgeni wa nchi za nje aliyehudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Rais huyo.

Sauti kutoka #PowerBreakfast nimeisogeza kwako hapa chini ndani yake utaweza kusikiliza uchambuzi wote wa magazeti.


PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments