Magazeti

Rais JPM na dawa za kulevya, Zitto na wanaompinga Rais JPM, Wabunge na mikopo? #PowerBreakfast.

on

Good Morning mtu wangu, Uchambuzi wa magazeti redioni @CloudsFM umekupita? Kazi yangu siku zote ni kuhakikisha zile zote kubwa za siku zinakufikia, hizi ni baadhi ya stori zilizoguswa kwenye Uchambuzi redioni.

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema wale wote wanaompinga Rais Dk. John Magufuli wana maslahi binafsi na mafisadi… Vyombo vya Ulinzi na Usalma vimeombwa kuongeza Ulinzi kwa Rais Dk. John Magufuli ambaye ametangaza wazi kupambana na mtandao wa wafanyabiashara wa dawa ya kulevya nchini.

Wabunge wagomea mkopo wa shillingi milion 90 wa kununulia magari yao, wanataka walipwe shillingi milion 130 ambayo ndio bei ya sokoni ya kununulia magari hayo kwa sasa… Masharti ya viongozi wa Serikali kusafiri nje ya nchi yawekwa wazi, kashfa nzito yaikumba manispaa ya Moshi baada ya TAKUKURU kugundua utata wa mkataba wa kampuni iliyoshinda zabuni ya mradi wa taa za barabarani.

Uchunguzi wa awali ya ajali ya Choppa ya Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe waonyesha chanzo kikuu cha ajali hiyo ni hitilafu ya engine… NECTA yasema ili kutekeleza sera ya elimu ya mwaka 2014, watoto wataanza kukariri darasa kuanzia darasa la pili, hatua hiyo itachukuliwa ikiwa tu watashindwa mtihani wa kujipima ambao utaanza rasmi mwakani kwa wanafunzi wa ngazi hiyo ya elimu.

SUMATRA yaanza kudhibiti nauli kwa msimu wa sikukuu wa Christmas na Mwaka Mpya, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amewaagiza uongozi wa mamlaka ya maji safi na taka Dar es salaam, DAWASA kuandaa orodha ya wananchi waliojenga nyumba juu ya miundombinu ya maji.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FBYOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments