Magazeti

Bajeti ya mwisho TZ.. Kingine kuhusu Uchaguzi Mkuu 2015 na kura ya Maoni ya Katiba.. Tukio la ujambazi DAR, Moshi >>StoriKubwa

on

elections_afrique_3Nimekusogezea hizi headlines karibu na wewe mtu wangu.. Uchambuzi wa MAGAZETI ya April 22 2015 umefanyika kwenye radio, nimerekodi na kukuwekea hapa pia.

Iko stori ya Bajeti ya mwisho kwa Serikali ya awamu ya nne kuanza kujadiliwa April 27, NEC imesema kuna uwezekano kura ya maoni ikafanyika pamoja na uchaguzi mkuu October 2015, Dr. Slaa amesema wamegundua NEC imeanza kuandikisha wapiga kura kwenye mikoa ambayo ni ngome ya CCM, nyingine inahusu mlinzi wa Askofu Gwajima kujisalimisha Mahakama ya Kisutu.

Kuna kichwa cha habari nyingine iliyoandikwa raia 12 wa Iran na Pakistan wanaokabiliwa na kesi ya kuingiza mihadarati TZ kuchoshwa na kesi yao kuchukua muda mrefu, kingine ni tukio la Polisi Dar kuwakamata watuhumiwa wanne waliofanya tukio la uporaji, Moshi kuna stori pia ya gari la kiwanda cha Bonite kuvamiwa na wafanyakazi wawili kuuawa.

Ishu ya madereva wa mabasi na malori nayo imerudi kwenye vichwa vya habari; wamesema wanasikitishwa na Serikali kushindwa kufanya nao mazungumzo na kutekeleza madai yao.

104.1 Clouds FM inasikika ukiwa Bukoba.

Hii imesikika kwenye PowerBreakfast @CloudsFM, bonyeza play kusikiliza…

millardayo.com ni sehemu yako utakapozipata zote unazozitaka, vichekesho, stori za siasa, muziki, michezo, movies, magazeti, video mpya na nyingine kubwa….  unaweza kujiunga na mimi Facebook, Twitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>>twitter Insta Facebook

Soma na hizi

Tupia Comments