Magazeti

Kauli ya Mkapa, Lowassa na style mpya ya kampeni, + Hofu ya mvua za El Nino DAR. (Audio)

on

leeo

Uchambuzi wa magazeti @CloudsFM umekupita? Jukumu langu ni kuhakikisha zile zote zinazoweka headlines magazetini kila asubuhi zinakufikia…

Mgombea Urais kupitia CHADEMA Edward Lowassa aanza kampeni kwa style ya kipekee kwa kupanda daladala kwa nia ya kusikiliza kero zinazowakabili madereva na makondakta kwenye usafiri wa uma… Mgombea Urais kupitia CCM John Magufuli asema kwenye safari yake ya kampeni atatumia usafiri wa barabara ili kuzijua kero za wananchi kwa ukaribu.

Kauli ya Benjamin Mkapa yazua mjadala, Rais za Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein achukua fomu ya ugombea Urais kupitia Chama Cha CCMNEC yawashukia CHADEMA... Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani ya Nchi Lawrence Masha akamatwa na kuwekwa rumande baada ya kujaribu kuwawekea dhamana vijana 17 wajulikanao kama 4U Movement.

Hali ya Kipindupindu jijini Dar es salaam yazidi kuwa tete idadi ya wagonjwa yafika 83 kwa wilaya za Temeke na Ilala… Mkurugenzi wa mamlaka ya hali wa hewa nchini asema nchi za Africa Mashariki zipo kwenye hati hati ya kukumbwa na mvua kubwa za El Nino miezi ya September mpaka December kutokana na joto kubwa.

Sauti yote ya uchambuzi wa magazeti kupitia #PowerBreakfast nimeisogeza kwako hapa chini.


PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments