Good Morning mtu wangu… leo ni Alhamisi 26 November 2015, na kama kawaida lazima asubuhi ianze na uchambuzi wa magazeti @CloudsFM. Kama ulipitwa nakukutanisha na hizi kwenye uzito wake !!
Serikali imesitisha maadhimisho ya siku ya UKIMWI na kuagiza fedha zote ambazo zilitengwa kwa ajili ya sherehe hizo zitumike kununua dawa kwa ajili ya waathirika wa UKIMWI… Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda awaweka rumande Maafisa 10 wa Ardhi kwa zaidi ya saa sita baada ya maafisa hao kuchelewa kufika katika ziara ya kutatua migogoro ya Ardhi Dar es salaam.
Utekelezaji wa ahadi za Rais Dk. John Magufuli zinazidi kushika kasi baada ya kuanza kwa mchakato wa kuanzisha Mahakama maalum ya kuwashughulikia mafisadi, Jaji Kiongozi Shaban Lila amesema wadau mbalimbali wameanza kukutana kuona namna ya kuanzisha Mahakama hiyo ikiwa ni sehemu ya kutekeleza ahadi za Rais Magufuli.
Kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi iliyofunguliwa na aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini kupitia chama cha NCCR Mageuzi, David Kafulila kupinga matokeo ya Uchaguzi itaanza kusikilizwa leo na Jaji John Utamwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora.
Gavana mmoja Kenya ajikuta matatani baada ya kutumia zaidi ya Milion 200 za Kikenya kutoka kwenye mfuko wa Serikali kwa ajili ya kuhudhuria Sherehe za kuapishwa kwa Rais Dk. John Magufuli, tarehe 5 November 2015.
Unaweza ukasikiliza uchambuzi wote wa magazeti kwenye #PowerBreakfast kwenye hii sauti hapa chini.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE