Umeamkaje mtu wangu? Kama ulipitwa na uchambuzi wa magazeti redioni @CloudsFM, hizi ni dakika 19 za Kuperuzi na Kudadisi leo November 27 2015, kama zilikupita hizi ni baadhi ya stori zilizogusa headlines asubuhi hii.
Viongozi wa dini ya Kiislamu wamepongeza hotuba na utendaji kazi wa Rais ya awamu ya tano, Rais Dk. John Magufuli na kutaka watendaji wake kutokumuangusha, pia kuwataka viongozi wa vyama vya Siasa kuepuka kukuza migogoro midogo bali wakae katika mazungumzo kujadili namna ya kuwaepuka wasioitakia mema nchi.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue amepiga marufuku utengenezaji na uchapishaji wa kadi za sikukuu za Christmas na Mwaka Mpya kwa kutumia gharama za Serikali/umma kwa mwaka huu, badala yake kuagiza fedha zilizotengwa kwa kazi hiyo zitumike kupunguza madeni ambayo Wizara na Idara na Taasisi za Umma zinadaiwa na wananchi.
Rais Dk. John Magufuli amerejea Dar es salaam na wakati wowote kuanzia sasa anaweza kutangaza Baraza la Mawaziri, Mkuu wa Mkoa Dar es salaam, Said Meck Sadick asema hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wale wote watakaokaidi agizo la Rais Magufuli la kufanya usafi siku ya Uhuru Tanzania bara, December 9 2015.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza awataka wakazi wa Tarafa ya Magoma waache kulima bangi na kulifanya zao hilo zao la biashara, badala yake awataka wakazi hao kuwekeza nguvu kwenye kulima mazao mengine kama mahindi, ufuta, na maharagwe.
Sauti yote ya uchambuzi wa magazeti kwenye #PowerBreakfast ipo hapa chini, kusikiliza bonyeza play ikupeleke moja kwa moja.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE