Taratibu za vijana wengi waishio kwenye mipaka ya nchi huwa ni pamoja na kujishughulisha na biashara za magendo ambazo zimekua zikipigwa vita na mataifa mbalimbali,Naibu waziri wa fedha Mwigulu Nchembe leo February 04 katika ziara yake ametembelea mto huo unaotenganisha Tanzania na Malawi.
Mto Songwe ni mto unaotenganisha Mpaka wa Tanzania na Malawi uliopo Wilayani Kyela Mkoani Mbeya,mto huu umeelekea hadi Ziwa Nyasa na ndio Mpaka wa Tanzania na Malawi,ingawa sehemu kubwa ya Mto umekua na vipenyo visivyo rasmi vinavyotumika na Wananchi Kuvusha Biashara za Magendo na Kukwepa kulipa kodi kwa kupita kwenye Kivuko rasmi cha Kasumulu kilichopo Kyela.
Wilaya ya Kyela pekee imetajwa kuwa na Vipenyo visivyo rasmi 32 vinavyotumika kupitisha bidhaa za magendo ikiwemo sukari, Viroba,Mpunga n.k,Katika hali ya kuonesha kuwa biashara ya Magendo imeshamili mpakani hapo,Naibu huyo Waziri wa Fedha ameshuhudia vijana wakivusha Sukari kutoka Malawi kuja Tanzania kwenye kipenyo kisicho rasmi kinachojulikana kwa jina la Timotheo
Miongoni mwa sababu walizotoa baada ya kuhojiwa Watanznaia hao wamesema wanalazimika kutumia njia hizo za panya kuvusha bidhaa hizo kwasababu ya Ushuru kuwa Mkubwa na Mtaji wao ni mdogo na kudai Ugumu wa Maisha ndio unawafanya wakimbilie kutafuta faida ya haraka ilikusaidia familia zao.