AyoTV

AUDIO: Rais Magufuli ‘huyu Shetani aliyetulaani Watanzania kwanini asife?’

on

Ni hotuba ya Rais Magufuli akiwa Arusha kwenye kuweka baraka zake kwenye majengo mapya ya PPF ambapo kwenye hotuba yake iliyochekesha watu wengi aliongelea pia ishu ya madini ya Tanzanite yanayopatikana Tanzania pekee lakini nchi zinazotambulika kuyauza duniani ni India na Kenya.

President Magufuli alisema >>>Siku nyingine hakuna ubaya hata NSSF mkawa ndio wawekezaji wakubwa wa Tanzanite mkawa mnanunua Tanzanite kutoka kwa vijana hawa badala ya kuwa inavushwa mpaka Kenya na kwenda Kenya, badala ya Tanzania kuwa ya kwanza kuuza Tanzanite duniani inajitokeza India alafu inafata Kenya

Unajua saa nyingine watu wanatuona Watanzania sijui tukoje, huyu shetani aliyetulaani sisi Watanzania kwanini asife? hata hatuhurumii kidogo? basi kama ni kuswali na kusali tusali sana ili tubadilike, tuthamini mali yetu kwa ajili ya vizazi vyetu

Kumsikiliza zaidi unaweza kubonyeza play hapa chini…

ULIKOSA? Kilichomchekesha Rais Magufuli japokua alikua kavaa sura ya kazi? tazama hii video hapa chini

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments