Habari za Mastaa

Magix Enga aliesababisha video ya 6ix9ine kuondolewa Youtube amsamehe

on

NI Headlines za Mtayarishaji wa muziki kutokea nchini Kenya aitwae Magix Enga ambae  ameingia tena kwenye vichwa vya habari baada ya kusababisha kuondolewa kwa video ya rapper wa Marekani aitwae  Tekashi 6ix9ine, ‘Gooba’ kupitia mtandao wa Youtube

Mtayarishaji huyo alimshtumu msanii huyo wa Marekani kuwa amesample mdundo wake na shtuma hizo zikawafikia Youtube kisha waliiondoa baada ya kupokea ripoti hiyo.

Miongoni mwa mitandao maarufu nchini Marekani iliyoandika taarifa hiyo ukiwemo  XXL uliripoti kuwa  video ya Tekashi 6ix9ine,  iitwayo ‘Gooba’  imeondolewa Youtube baada ya Mtayarishaji kutokea Kenya Megax Enga kuwa amewasilisha madai yake ameibiwa kazi yake

Huu ndio muonekano wa video ya 6ix9ine baada ya Megix Enga kuwasilisha madai yake kuibiwa na ukiifungua video hiyo inakuandika hivyo

Sasa leo Magix Enga kupitia ukurasa wake wa instagram leo amepost video ikimuonesha akizungumza maneno yanayoashiria kumsamehe Rapper huyo wa Marekani na video hiyo ikarudishwa hewani

Soma na hizi

Tupia Comments