fB insta twitter

Simu bandia zapata soko

on

Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter>>>@millardayo na Zote nakusogezea hapa chini.

Moja ya habari iliyoripotiwa ni hii kutoka gazeti la Mwananchi, yenye kichwa cha habari ‘simu bandia zapata soko Msumbiji, Congo’.

Gazeti hilo limeripoti kuwa Siku mbili baada ya mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kuzima simu feki, wafanyabiashara wa simu hizo wamepata soko jipya katika nchi za Msumbiji na Congo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hilo, baadhi ya vijana waliokutwa wakizunguka madukani kuzikusanya, walisema wanazinunua na kuzisafirisha kwenda huko kwa ajili ya kuziuza kwa watumiaji. Walisema katika nchi hizo kuna soko kwa sababu zinakamata mawasiliano kama kawaida.

Gazeti hilo limemnukuu Lawrence Kyondo ambapo amesema wanazinunua kwa bei ya makubaliano na kwenda kuziuza katika soko la nje……….>>>’hatujaanza hii biashara leo, siku nyingi isipokuwa wenye maduka walikuwa bado wagumu kuziuza wakidhani hazitazimwa’

Unaweza kuzipitia habari zingine kubwa kwenye magazeti ya leo hapa chini

UMEKOSA KUANGALIA UCHAMBUZI WA MAGAZETI JUN 19 2016 KUTOKA AYO TV? UNAWEZA KUTAZAMA VIDEO HII HAPA CHINI

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments