AyoTV

VIDEO: ‘Hakuna mtu anataka kumjaribu Rais Magufuli, mahabusu sio pazuri’ -Tundu Lissu

on

August 9 2016 Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekutana na waandishi wa habari Dar es salaam kutoa taarifa kwa umma kuhusu madai ya vitisho wanayoyapata baada ya kutangaza kufanya maandamano ya nchi nzima.

Mwanasheria wa chama hicho Tundu Lissu amesema>>>’Hakuna mtu anataka kumjaribu mtukuru Rais na wala hakuna anayetaka kukamatwa na Polisi, mahabusu sio pazuri niwaambieni mimi ambaye nimekuwamgeni wa dola mara mbili katika mwezi uliopita‘ –Tundu Lissu

Tunachotaka kukifanya ni ambacho kipo katika katiba, mikutano na maandamano ya kisiasa kwakuwa ni halali. Kama kufanya hivyo Rais Magufuli anafikiri tunamjaribu hayo ni mawazo yake‘ –Tundu Lissu

ULIIKOSA HII YA TUNDU LISSU ALIVYOFIKISHWA MAHAKAMANI KUJIBU TUHUMA ZA UCHOCHEZI

Soma na hizi

Tupia Comments