Mix

Uteuzi mwingine aliofanya Rais Magufuli

on

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anazidi kuendelea kuisuka Serikali yake ili iwe yenye ufanisi zaidi. Leo March 19 amefanya uteuzi ambao umeziba baadhi ya nafasi zilizokuwa wazi. Rais Magufuli amefanya uteuzi wa watendaji wakuu wa Taasisi tatu za serikali kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo. 

Rais Magufuli amemteua Profesa Godius Kahyarara kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF). Prof. Kahyarara anachukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Ramadhan Dau, ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.

Aidha Rais Magufuli amemteua Dkt. Ayub Rioba Chacha kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC). Dkt. Rioba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Clement Mshana ambaye amestaafu.

Rais  Magufuli amemteua pia Dkt. Mussa Iddi Mgwatu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hodhi ya rasilimali za reli Tanzania (RAHCO). Dkt. Mgwatu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhandisi Benhadard Tito, ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Unataka kutumiwa za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana naMillardAyo kwenyeTwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE

Uliikosa video ya kilichomchekesha Rais Magufuli japokuwa alikua kavaa sura ya kazi IKULU? Angalia video hii hapa chini.

Soma na hizi

Tupia Comments