Imeelezwa kuwa Magonjwa yasioambukiza yamekuwa changamoto kubwa sana katika Bara la Afrika ikiwemo ugonjwa wa Kisukari huku ikisemwa ya kuwa Ugonjwa huo Umegawanyika katika Sehemu Tatu, Pamoja na Shinikizo la Damu .
Hayo Ameyasema Daktari Bingwa wa Magonjwa Yasioambukiza Dkt. Mlawa Maneno katika siku ya kuadhimisha wiki ya Ugonjwa wa Kisukari ambapo Hospitali ya Apolo iliyopo Jijini Dar es salaam walifanya kwa kuwapatia Vipimo, Tiba pamoja na Elimu Bure juu ya Magonjwa yasioambukiza .
Hata hivyo Dkt. Mlawa Amewataka Watanzania kujitahidi Kujitokeza Katika Vituo Vya Afya kwa lengo la Kujua Afya Zaidi Pamoja na Kusisitiza Kuzidisha Mazoezi walau Kwa Wiki Mara 3 ili kupunguza magonjwa yasioambukiza .