Premier Bet
TMDA Ad

Duniani

PICHA 10: Adhabu za Ulaya kwa Madereva wanaopaki magari vibaya

on

Kwa Tanzania gari yako ikikutwa imewekwa sehemu isiyotakiwa sanasana wataipiga pini kwa minyororo au kuibeba na wewe utaikuta Manispaa kwa ajili ya kulipia faini ila kwa wenzetu Ulaya inawezekana tumetofautiana kidogo na ndio maana nimekukusanyia hizi picha 10 za adhabu kwa waliopaki vibaya.

Huyu Jamaa baada ya kupaki vibaya alikuta gari lake limezungushiwa kama hivi ili akome.

Kwenye nchi za Wenzetu miji imepangika kiasi kwamba mabomba ya maji ya kuzimia moto huwa yanawekwa mtaani ili kurahisisha kazi moto ukitokea ambapo huwa ni marufuku kupaki gari karibu na bomba hilo, sasa kilichomkuta huyu jamaa ni Zimamoto kuvunja Vioo vya gari lake ili waweze kupitisha bomba.

Huyu Jamaa aliwekewa vizuizi baada ya kupaki katikati ya barabara.

Huyu Jamaa baada ya kupaki vibaya alikuta gari lake limewekewa uchafu ili akome siku nyingine.

Huyu alikuta amewekewa tuzo ya kuwa dereva mbovu zaidi duniani.

Baada ya kupaki vibaya alikuta madebe ya takataka ili kumuonesha jinsi gani ni dereva mbovu.

Baada ya kupaki vibaya alikuta magari mawili yamemzuia kutoka ili siku nyingine asirudie tena.

VIDEO: Kutana na Jamaa anaesifiwa kwa kumuigilizia sauti Mstaafu Jakaya Kikwete, bonyeza play kwenye hii video hapa chini

BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo

Soma na hizi

Tupia Comments