fB insta twitter

TCU yatoa ufafanuzi kuhusu taarifa za kufungiwa vyuo 22 zilizosambaa

on

Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.

Moja ya yalioandikwa ni huu utafiti wenye kwenye gazeti la Jambo leo yenye kichwa ‘TCU: Hakuna vyuo vilivyofungiwa ”

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imewatoa hofu wanafunzi waliohitimu katika vyuo vilivyozuiwa hivi karibuni kufanya udahili, huku ikikanusha taarifa za kuzifungia udahili wa kozi tofauti vyuo 22 zilizozagaa juzi.

Hivi karibuni TCU ilitangaza kusimamisha kufanya udahili  vyuo vitano baadhi vikiwamo Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Chuo Kikuu cha Mtakatifu Francis cha Ifakara Morogoro, Chuo cha Mtakatifu Joseph cha Dar es Salaam na Chuo cha IMTU cha Dar es Salaam vyote kwa kozi ya udaktari.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana, Kaimu Katibu Mtendaji wa TCU, Eliuther Mwageni alisema kufungiwa kwa vyuo hivyo ni kwa muda mpaka vitakapokabidhi vigezo vinavyotakiwa.

Mwageni alisema…….>>>”Kuna vigezo vinavyotakiwa kufikiwa ili chuo kiweze kusajiliwa  na hivi vyuo hatujavifungia ila tumevisimamisha kwa muda mpaka vikidhi vigezo vyetu.

Kuhusu taarifa za vyuo 22 kusimamishwa kudahili wanafunzi katika kozi mbalimbali zilizozagaa kwenye mitandao juzi na jana, Mwageni alisema……>>> ‘taarifa hizo ni za uzushi, zina lengo baya hivyo hazina ukweli wowote‘.

Source: Gazeti la Jambo Leo

ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI JULY 26 KUTOKA AYO TV UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments