Mix

PICHA 6: Rais Magufuli alivyokutana na kiongozi wa chama cha kikomunisti China

on

June 04 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amewaalika wawekezaji kutoka Jimbo la Jiangsu la nchini China kuungana na Tanzania katika utekezaji wa mpango wa ujenzi wa viwanda na ujenzi wa miundombinu hususani reli na amewahakikishia kuwa serikali yake ya awamu ya tano itatoa ushirikiano wa karibu kufanikisha uwekezaji huo.

>>>.”Mheshimiwa Luo Zhijun naomba uwaeleze wafanyabiashara wa Jimbo lako la Jiangsu kwamba ninawakaribisha kwa mikono miwili, waje hata kesho waseme wanataka kuanzisha kiwanda gani na sisi tutawapa ushirikiano”.

>>>”Tunayo maeneo ya kutosha ya kuanzisha viwanda, kwa Pwani na Dar es salaam tuna eneo la Bagamoyo tunaloweza kuweka viwanda zaidi ya 1,000 halikadharika Kigamboni na maeneo mengine mengi katika mikoa mbalimbali nchini nzima” :- Rais Magufuli

Kwa upande wake Luo Zhijun amemshukuru Rais Magufuli kwa utayari wake wa kuwapokea wawekezaji kutoka Jimbo la Jiangsu na amemuahidi kuwa pamoja na kwamba Jimbo hilo tayari limewekeza hapa nchini kiasi cha dola za Marekani Bilioni 1 (Sawa na Shilingi Trilion 2.2) atahakikisha anawashawishi wawekezaji wengi zaidi wa viwanda katika jimbo lake

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ambaye June 03 2016 ametiliana saini makubaliano ya ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Mkoa wa Dar es salaam na Jimbo la Jiangsu ambapo jimbo hilo limeahidi kuwekeza katika miradi mbalimbali ya viwanda vya mazao ya kilimo, ujenzi na huduma za kijamii.

4 6 7 8 9 10

ULIKOSA HII KAULI YA RAIS MAGUFULI KUHUSU MSAADA WA CHINA KUWA HAUNA MASHARTI? BONYEZA PLAY HAPA CHINI

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments