Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli , leo mchana amefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kukutana na hali ya kumsikitisha.
Rais huyo wa awamo ya tano alipofika katika hospitali ya Muhimbili amekasirishwa na hali ya kutokujali wala kushughulikia vifaa vya kufanyia kazi ambapo amekuta mashine muhimu za uchunguzi wa magonjwa kama vile MRI na CT-SCAN zikiwa hazifanyi kazi kwa muda wa miezi miwili sasa, ilihali mashine kama hizo katika Hospitali za binafsi zinafanya kazi na wagonjwa wanaelekezwa kwenda kutafuta huduma huko.
‘Tatizo la hospitali za serikari mnaharibu vifaa ili vikafanye kazi kwa watu binafsi, vifaa vya hospitali za private zinafanya kazi lakini za hapa Muhimbili hazifanyi kazi…! Na watu wanasafiri kwenda Ulaya, Mungu atawalipa‘-RAIS Dk.MAGUFULI
‘Mpelekeni akafanyiwe matibabu na mimi nitatoa hata mshahara wangu kumlipia, haiwezekani akakaa mwezi mzima..! na nitalifuatilia’ – Rais DK. MAGUFULI
Nimekuwekea hapa chini sauti yote, waweza kubofya kwa kuisikiliza…
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM, TWITTER, FB, YOUTUBE