Top Stories

Magufuli afichua Mtoto wake kuumwa Corona “kajifungia, kajifukiza kala malimao” (+video)

on

Rais Mmagufuli leo akihutubia Mkoani Geita “Mimi Mtoto wangu wa kumzaa amepata corona akajifungia, akajifukiza akapiga malimao, sasa hivi ni mzima kabisa anapiga push-up, msije mkadhani mimi sijapata Mtu wa karibu mwenye corona, tuondoe hofu”-JPM

“Kuna mambo ya hovyo yanafanyika, kila Mtu akifariki wanakimbilia kumpima corona, Mtu amefariki unampima yanini?, nguvu za kumpima wanazo, za kumuhudumia akapona hawana, Mtu atakapofariki kwa ugonjwa wowote hata wa corona lazima azikwe kwa kawaida, corona sio Ebola” -JPM

“Kuna rafiki yangu mmoja Injinia alipata kiharusi akapelekwa Muhimbili, wakampima wakasema ana corona, amepelekwa Amana Watu wanamuogopa kisa ana corona, Ndugu zake wakamtoa wakampeleka Agha Khan, wamechukua vipimo wakakuta mzima hana corona, amepona yupo nyumbani” -JPM

SABABU YA RAIS MAGUFULI KUTOKUFUNGA MIPAKA YA NCHI

Soma na hizi

Tupia Comments