Top Stories

Magufuli apanda kiberenge, IGP Sirro, Mkuu wa Majeshi wakaa pembeni yake (+video)

on

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 28 Juni, 2020 amekagua maendeleo ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (standard gauge) kwa sehemu ya kwanza ya Dar es Salaam – Morogoro na kuelezea kuridhishwa kwake na maendeleo ya ujenzi wa mradi huo mkubwa.

Rais Magufuli amesafiri kwa gari kandokando ya reli hiyo kuanzia Kisarawe hado Soga Mkoani Pwani na kisha akapanda kiberenge kilichopita katika reli hiyo mpya kuanzia Soga hadi Kikongo kabla ya kuendelea na safari yake kwa gari kuelekea Morogoro.

HD VIDEO: “HUYU ANACHUKUA WAKE ZA WATU, NAMTUMBUA HAPA HAPA, HAFAI KUWA KIONGOZI”

https://youtu.be/7c0tskkixrc

Soma na hizi

Tupia Comments