fB insta twitter

‘Hashtag’ mpya ya Rais Magufuli ilivyokamata Twitter!

on

Utendaji kazi wa Rais Dk. John Magufuli umekuwa topic kubwa sana kwenye mitandao mbalimbali ya Tanzania na nchi za jirani… Mwanzoni nilikusogezea tweets za Wakenya zikimgusa Rais Magufuli kwenye kona mbalimbali za utendaji kazi wake ambazo nyingi zilikuwa za kumpongeza.

Leo nimechukua tena time ya kutembelea tena mtandao wa kijamii wa Twitter na huko nimekutana na ‘hashtag’ mpya ya Rais Magufuli, yenyewe inaitwa ‘#WhatWouldMagufuliDo’ (‘#MagufuliAngefanyaNini’) ambayo kuanzia jana ilianza kuweka headlines kwenye twitter kutokana na matumizi yake!

HASH3

Kazi yangu ni kukisogeza chochote kile ninachokipata  mtu wangu, na leo napenda nishare na wewe hizi Tweets ambazo pengine mpaka sasa hivi hujafanikiwa kukutana nazo… watu mbalimbali ikiwemo wasanii wa muziki kama Vanessa Mdee, Sauti Sol na Wakazi wamechukuwa time na kuitumia hashtag hii mpya, ila nyingi nilizokutana nazo zitakufuraisha.

Hizi hapa ni tweets 15 za #WhatWouldMagufuliDo nilizofanikiwa kuzinasa:

HASH1

>>> “Nilitaka kununua dawa ya malaria lakini nikawaza #WhatWouldMagufuliDo“. <<< @AbbyKirahi.

HASH8

>>> “#WhatWouldMagufuliDo kwa ajili ya ushindi“. <<< @VanessaMdee.

HASH10

>>> “Pale ambapo baby anataka kula nje na kupata romantic dinner na mshumaha lakini unajiuliza #WhatWouldMagufuliDo“. <<< @WOAT.

HASH9

>>> “Nilitaka kuachia single moja lakini nikawaza #WhatWouldMagufuliDo na sasa nimedondosha single 2 mpya & nyingine itadondoka wiki ijayo“. <<< @Wakazi.

HASH2

>>>”Pale ambapo Samaki Samaki wanakuambia Samaki ni 18,000/- na unaanza kuwaza #WhatWouldMagufuliDo“. <<< @AbbyKirahi.

HASH4

>>> “Nilitaka kwenda kwa kinyozi lakini nikawaza #WhatWouldMagufuliDo“. <<< @AbbyKirahi.

HASH16

>>> “Nilitaka kufunga DSTV nyumbani kwangu lakini nikawaza #WhatWouldMagufuliDo ! Star Times ndio mwisho wa mawazo saa hii“. <<< @Alawiabudl.

HASH12

>>> “Nilitaka kununua deodorant lakini nikajiuliza #WhatWouldMagufuliDo.. *pulizia air freshener ya ofisi*“. <<< @Dave.

HASH14

>>> “Nilikuwa natoka ATM bila kuhesabu hela zangu lakini nikawaza #WhatWouldMagufuliDo, kwahiyo bado nipo hapa nahesabu“. <<< @DennisWaithaka.

HASH18

>>> “Nilitaka nimpeleke mke wangu kwenye resort ZNZ lakini nikawaza #WhatWouldMagufuliDo kwahiyo nimejaza maji na chumvi bafuni kwangu, sasa tupo tunachill“. <<< @MahmudKullane.

HASH11

>>> “Nilitaka kununua Galaxy Note 5 lakini nikawaza #WhatWouldMagufuliDo kwahiyo nimeishia kununua simu hii“. <<< @Sammy.

HASH15

>>>”Girlfriend wangu alitaka pesa ya kununulia wanja, nikajiuliza #WhatWouldMagufuliDo; badala yake tumetumia marker pen za ofisini“. <<< @Dave.

HASH13

>>> “Nilitaka nimnunulie girlfriend wangu zawadi ya birthday lakini nikajiuliza #WhatWouldMagufuliDo kwahiyo nimeishia kununua mbolea na kumpeleka kijijini kulima“. <<< @WaKimuyu.

HASH19

>>> “Kabla hujatoa mchango mwengine wa harusi jiulize#WhatWouldMagufuliDo?” <<< @LatifAmars.

HASH5

>>>”Kifurishi chako cha DSTV kinapoisha lakini hutaki kupitwa na mechi, kwahiyo unajiuliza #WhatWouldMagufuliDo“. <<< @WOAT.

Kama una ya kwako ambayo ungependa kushare na mimi, feel free kuiacha hapa chini kwenye comment kwa kutumia #WhatWouldMagufuliDo hapa chini ili inifikie…

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments