Mix

Ushauri wa Rais Magufuli kwa Rais wa Uganda Yoweri Museveni

on

May 12 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amefanya mazungumzo na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni muda mfupi baada ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Rais huyo iliyofanyika katika uwanja wa Kololo Jijini Kampala.

Baada ya Rais Magufuli kutoa pongezi kwa Rais wa Uganda, viongozi hao wamezungumzia mradi mkubwa wa ujenzi wa bomba la mafuta la kutoka Hoima (Ziwa Albert) nchini Uganda hadi bandari ya Tanga ambapo pamoja na kuishukuru Uganda kwa uamuzi wake wa kuamua bomba hilo lipitie Tanzania.

Rais Magufuli amemshauri Rais Museveni kufupisha muda wa ujenzi wa mradi huo, kwa kutumia mbinu inayojumuisha usanifu na ujenzi (Design and Construct method) na kutumia wakandarasi wengi watakaogawanywa katika vipande tofauti badala ya kutumia mkandarasi mmoja.

>>>”Nashauri tutumie mbinu ya usanifu na ujenzi pamoja, hii ni njia ya haraka zaidi, na pia tugawe vipande vya ujenzi kwa njia yote ya bomba la mafuta yenye urefu wa kilometa 1,410 tunaweza kuwa na Wakandarasi watano mpaka sita ambao watatumia njia hiyo mpya ya usanifu na ujenzi.

>>>”Kwa kufanya hivyo tutakuwa tumepunguza muda utakaotumika kwa ajili ya ujenzi wa bomba la mafuta, inaweza hata kuchukua mwaka mmoja tu” :-Rais Magufuli.

Rais Magufuli amebainisha kuwa kwa kufanya hivyo faida za mradi huo wa mafuta zitaanza kupatikana mapema badala ya kusubiri miaka miwili au mitatu ijayo na kwamba hiyo itakuwa inaendana na kauli mbiu yake ya “Hapa Kazi Tu”

5

Rais Magufuli na Rais Museveni

Rais Magufuli amemshukuru Rais Museveni kwa uamuzi wa nchi hiyo wa kuipa Tanzania umiliki wa asilimia 8 katika mradi huo wa bomba la mafuta.

Kwa upande wake Rais Museveni amesema amefurahishwa na hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi huo, na pia amempongeza Rais Magufuli kwa juhudi zake kubwa ambazo amezifanya katika mapambano dhidi ya rushwa nchini Tanzania………..

>>>”Napenda kasi yako ya uongozi, napenda jinsi unavyopambana na rushwa, kwa sababu rushwa ilikuwa inazaa matatizo mengine kama vile ucheleweshaji wa mizigo bandarini na vikwazo vya mpakani, hivyo nakupongeza sana kwa hilo” 

1

ULIZIKOSA SABABU ZA BANDARI YA TANGA KUTEULIWA KUTUMIWA NA BOMBA LA MAFUTA  KUTOKA UGANDA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments