Ad

Mix

Kitu Rais Magufuli amemwambia Mkuu mpya wa Polisi Simon Sirro leo

on

Rais John Pombe Magufuli leo June 02 2017 kwenye bwalo la Polisi Osterbay Dar es salaam amezungumza na Makamanda Wakuu wa Polisi kutoka Makao makuu ya polisi, Makamanda wa Mikoa na Vikosi vya Tanzania Bara na Zanzibar pamoja na viongozi wote wakuu wa Polisi Dar es Salaam.

Kwenye kikao hicho kilichohudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba na Katibu Mkuu wa wizara ya mambo ya ndani ya nchi Meja Jenerali Mstaafu Projest Rwegasira, President JPM amemwambia Mkuu mpya wa jeshi la Polisi Simon Sirro asiangalie sura ya mtu.

Namnukuu akisema >>> ‘IGP fanya marekebisho ya Jeshi lako lote, usiangalie sura ya mtu wala nani yuko karibu na nani, fanya kwa ajili ya Jeshi la Polisi lirudishe nidhamu ya zamani, nawapenda sana Askari na nataka niwaambie ukweli, wale wachache wanawachafua mno

Rais Magufuli amelipongeza Jeshi la Polisi kwa juhudi zake za kukabiliana na uhalifu lakini ametaka juhudi hizo ziongezwe hususani kukabiliana na matukio ya ujambazi na mauaji ya raia, dawa za kulevya na kuendesha operesheni zenye tija katika mikoa yote.

Amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro kujipanga vizuri yeye na safu yake ya Makamanda, Viongozi Wakuu wa Vikosi na Maofisa mbalimbali ili kuondoa dosari zote za utendaji kazi zinazoshusha ufanisi na heshima ya Jeshi la Polisi.

“Ni lazima ufanye mabadiliko makubwa, nataka kuona Jeshi la Polisi linakuwa Jeshi la Polisi, Wewe IGP Sirro na Makamnda wenzako hakikisheni mnakomesha uhalifu, komesheni mauaji dhidi ya raia, ujambazi na dawa za kulevya” – Rais Magufuli.

Vilevile President amewataka Makamanda, Maofisa na Askari wa jeshi hilo kujiepusha na rushwa, dawa za kulevya, kutumiwa na watu kwa maslai binafsi, kuingia mikataba isiyo na maslai kwa Jeshi na Taifa, ubadhirifu na kuacha upendeleo katika utoaji wa ajira na vyeo.

Kwa kumalizia pia ametaka Makamanda, Maofisa na Askari wote wa Jeshi la Polisi wampe ushirikiano wa kutosha IGP Simon Sirro ambaye hivi karibuni amemteua kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.

ULIPITWA? Yote yaliyosemwa na Rais Magufuli June 1 2017 yako hapa chini kwenye hii video

Soma na hizi

Tupia Comments