Taarifa kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu imetoa taarifa ya Rais John Magufuli kuwateua mabalozi watano watakaokwenda kuiwakilisha Tanzania kwenye nchi mbalimbali.
Katibu Mkuu kiongozi Balozi John Kijazi amewataja Mabalozi walioteuliwa pamoja na vituo vyao vya kazi…
1.Balozi Mbelwa Brighton Kairuki ambaye ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania Beijing – China
2.Balozi George Kahema Madafa ambaye yeye ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania Rome – Italy.
3. Balozi Emanuel John Nchimbi ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania Brasilia – Brazil.
4. Balozi Fatma M Rajabu ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania Doha – Qatar.
5. Balozi Prof. Elizabeth Kiondo ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania Ankara – Uturuki.
6. Balozi Dkt. James Alex Msekela ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania Geneva – Umoja wa Mataifa.
Kwenye taarifa nyingine Rais Magufuli amemteua Muhidin Ally Mboweto kuwa Balozi,tarehe ya kuapishwa na kituo chake cha kazi itatangazwa baadae.
ULIPITWA? Rais Magufuli alivyotumia dakika zake 16 kutoa tathmini ya uongozi wake? bonyeza play kutazama hii video hapa chini