Mix

PICHA 10: Rais Magufuli alivyotua nchini Uganda leo May 11 2016

on

Leo May 11 2016 Rais Magufuli ameingia tena kwenye headline ambapo taarifa zinasema mapema leo Rais Magufuli ametua nchini Uganda ikiwa ni safari yake ya pili kwenda nje tangu aingie madarakani.

Rais Magufuli amewasili Jijini Kampala nchini Uganda ambapo kesho anatarajiwa kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Jamhuri ya Uganda Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni.

Rais Magufuli ametua katika uwanja wa ndege wa Entebe majira ya saa tano za asubuhi na kupokelewa na Waziri wa Ujenzi na usafirishaji wa Uganda Mheshimiwa John Byabagambi na kisha kuelekea Ikulu ya Entebe ambako amepokelewa rasmi na mwenyeji wake Rais Yoweri Kaguta Museveni.

Akiwa katika Ikulu ya Entebe Rais Magufuli amekagua gwaride rasmi lililoandaliwa kwa heshima yake na pia amepigiwa mizinga 21, aidha Viongozi hao wamefanya mazungumzo ambapo pamoja na kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano na uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Rais Magufuli amemhakikishia Rais Museveni kuwa Tanzania itatoa ushirikiano wa kutosha kufanikisha ujenzi wa bomba la mafuta linalotarajiwa kujengwa kutoka Hoima katika Ziwa Albert nchini Uganda na kupita kaskazini mwa Tanzania hadi bandari ya Tanga.

1

Rais wa Tanzania john Magufuli na Rais wa Uganda Yoweri Museveni

3...

.

3..

.

2

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

ULIKOSA HOTUBA YA KWANZA YA RAIS MAGUFULI NJE YA NCHI NCHINI RWANDA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments