Ad

Mix

Manne aliyoyazungumza Rais Magufuli April 21 2016, wanaotumbuliwa hadharani, watumishi hewa, Bandari na CCM

on

April 21 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amekutana na wenyeviti, makatibu wa chama cha mapinduzi ‘CCM’ wa mikoa na wilaya za Tanzania na visiwani Ikulu jijini Dar es salaam kwa ajili ya kutoa shukrani.

Katika mambo aliyoyazungumzia Rais Magufuli ni hii ya kituo cha haki za binadamu kukosoa aina ya utumbuaji majipu hadharani kuwa ni udhalilishaji na kinyume cha sheria, hapa Rais Magufuli amelizungumzia hilo……..

>>>’wanasema tunawanyanyasa sijui haki za binadamu eti kwa sababu tunawatangaza hadharani kwa hiyo wao walikuwa na haki mno kuwaibia hadharani watanzania, waliwaibia watanzania hadharani lazima tuwatangaze hadharani, mateso waliyoyapata watanzania mamilioni kwa sababu za kuibiwa na hawa wachache lazima na wao waanze kupata hayo mateso’:-Rais Magufuli

>>’kwa hiyo unaweza kuona hawa wanaowatetea nao ni majipu nao tutaanza kuwafuatilia, lakini kwa bahati nzuri aliyewateua ni mimi na niliwataja hadharani kwa hiyo kwa nini wafurahi siku ya kuteuliwa na wasitajwe hadharani siku ya kutumbuliwa’:-Rais Magufuli

Aidha Rais Magufuli ameligusia suala la watumishi hewa……..>>>’mpaka leo wafanyakazi hewa tuliowatoa kwenye register wamezidi 7700 na bado uchambuzi unaendelea sasa mnaweza mkaona kama kuna wafanyakazi hewa wa namna hiyo ndani ya serikali, hayo mabilioni ya fedha yangeweza kwenda kwenye huduma mbalimbali;-Rais Magufuli

Ameligusia pia suala la stori zilizoenea kuwa mizigo imepungua bandarini kwa sasa…….>>>’iliyopungua ni ya wale waliokuwa wanaingia bila kulipa kodi, na wale waliokuwa hawalipi kodi wasije, nafuu uwe na mizigo michache ya watu walio commited kulipa kodi‘:-Rais Magufuli

>>>’nataka kuwahakikishia ndungu zangu wana CCM nchi itakwenda na bahati nzuri sasa hivi tumeanza kupata support kubwa sana kwa wafadhili hakuna mfadhili anayependa watu wa kwao huko walipe kodi halafu nyie mzitumie vibaya, baada ya hatua hizi tulizozichukua kila mmoja anasema analeta fedha’:-Rais Magufuli

Rais Magufuli akamalizia kwa kuwaomba viongozi wa CCM kusahau yaliyopita na kuwa pamoja>>>’niwaombe tu viongozi wenzangu wa chama cha mapinduzi kwa sababu sasa hivi kampeni zimeisha na nimesema yaliyopita sio ndwele, tulifikia mahali kwa kutoaminiana na tukishajenga tendecy ya namna hiyo tutakuwa tunakiua chama’:-Rais Magufuli

UNAWEZA KUSIKILIZA DAKIKA 5 ZA RAIS MAGUFULI KUWAJIBU WANAOSEMA ANANYANYASA KWA KUTUMBUA MAJIPU HADHARANI, BONYEZA PLAY HAPA CHINI

ULIIKOSA VIDEO YA KILICHOMCHEKESHA RAIS MAGUFULI JAPOKUWA ALIKUA KAVAA SURA YA KAZI? ANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments