AyoTV

VIDEO: Rais Magufuli alivyofanya ziara ya kushtukiza Wizara ya maliasili na utalii

on

October 29 2016 Rais John Pombe Magufuli alifanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za Wizara ya maliasili na utalii (Mpingo House) kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa operesheni ya kukabiliana na ujangili inayofanywa na Kikosi Kazi kilichoundwa na wizara hiyo ambapo ameshuhudia pembe 50 katika siku mbili za jana na leo.

Rais Magufuli pia amewapongeza askari wote waliopo katika Kikosi Kazi cha kudhibiti na kupambana na biashara haramu ya pembe za ndovu pamoja na raia wema wote wanaotoa ushirikiano katika operesheni hiyo na amewahakikishia kuwa anatambua kazi kubwa wanayoifanya na anawaunga mkono.

Nawapongeza sana kwa kazi nzuri mnayoifanya na ninawahakikishia kuwa ninawaunga mkono, chapeni kazi, wakamateni wote wanaojihusisha na biashara hii haramu, hakuna wa kumbakiza, awe mkubwa au nani, kamateni, wala msijali cheo chake, umri wake, dini yake, kabila lake, umaarufu wake‘ –Rais Magufuli

Sheria ni msumeno, watafuteni wote mpaka watu wakiona tembo wawe wanakimbia wenyewe ili tuokoe wanyama wetu ambao wanaendelea kutekelezwa‘ –Rais Magufuli

Hapa mmekamata pembe 50 maana yake tembo 25 wameuwawa, haiwezekani maliasili yetu ikawa inapotea hovyo hovyo kwa sababu ya watu wachache wenye tamaa ya kutaka utajiri wa haraka haraka‘ –Rais Magufuli

ULIIKOSA HII TAARIFA YA IKULU KUHUSU RAIS MAGUFULI KUTENGUA UTEUZI WA MKURUGENZI

Soma na hizi

Tupia Comments