Mahakama ya Uchaguzi nchini Afrika Kusini jumanne wiki hii imeamua aliyekuwa rais wa nchi hiyo Jacob Zuma kugombea muhula mwingine katika uchaguzi utakaofanyika mwezi ujao, hatua inayobatilisha uamuzi uliomwekea kikwazo kiongozi huyo kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi huo.
Zuma atagombea nafasi ya urais kupitia chama cha uMkhonto weSizwe ama MK, chama kipya cha siasa nchini humo ambacho alijiunga nacho baada ya kujitoa uanachama wa chama chake cha zamani cha ANC.
Awali, Tume Huru ya Uchaguzi nchini humo ilimtengua Zuma kutogombea nafasi hiyo kwa mara nyingine kutokana na rekodi za uhalifu alizokuwa nazo rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini.
Afrika Kusini inatarajiwa kufanya uchaguzi wa viongozi wa kitaifa na serikali za mitaa Mei 29 mwaka huu.